Ijumaa 30 Januari 2026 - 09:00
Ikiwa Iran itapata madhara, ulimwengu wa Kiislamu utapata madhara makubwa zaidi

Hawza/ Maulawi Ibrahim Abdullah, Rais wa Jumuiya ya Sufi nchini Sri Lanka, katika kikao chake na mshauri wa masuala ya kitamaduni wa Iran nchini Sri Lanka, alisema: Tunaamini kuwa katika ulimwengu wa leo na miongoni mwa Umma wa Kiislamu, ni Iran pekee ambayo daima imekuwa ikiunga mkono Waislamu na maslahi yao; na kwa sasa ni lazima mataifa ya Kiislamu yasimame pamoja na wananchi wa Iran.

Kwa mujibu wa ripoti ya kiengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kufuatia njama za maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu za kusababisha machafuko na fitna nchini Iran, Maulawi Ibrahim Abdullah, Rais, pamoja na idadi ya wanachama wa Jumuiya ya Masufi wa Sri Lanka, katika kikao chao na Ali Kabriaei-Zadeh, mshauri wa masuala ya kitamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, walitangaza kuwaunga mkono wananchi wa Iran, Mapinduzi ya Kiislamu na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi.

Katika kikao hicho kilichofanyika katika ofisi ya mshauri wa masuala ya kitamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Sri Lanka, Maulawi Ibrahim Abdullah aliisifu subira na uthabiti wa wananchi wa Iran katika kukabiliana na njama za maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu, pamoja na busara ya uongozi kwa kusema: Katika mazingira kama haya, ni lazima Waislamu duniani waweke pembeni tofauti zao na kusimama pamoja, na wasiwaruhusu Marekani na Israel kufikia malengo yao ya kuchochea mifarakano miongoni mwa mataifa huru duniani.

Rais wa Jumuiya ya Masufi wa Sri Lanka, huku akisisitiza kwamba; iwapo Iran itapata madhara, ulimwengu wa Kiislamu utakumbwa na madhara makubwa zaidi, alisema: Tunaamini kuwa; katika ulimwengu wa sasa na miongoni mwa Umma wa Kiislamu, ni Iran pekee ambayo daima imekuwa ikiwaunga mkono Waislamu na maslahi yao; na kwa hiyo, leo ni wajibu wa mataifa ya Kiislamu kusimama pamoja na wananchi wa Iran.

Kwa upande wake, Ali Kabriaei-Zadeh, mshauri wa masuala ya kitamaduni wa Irani nchini Sri Lanka, alisema: Kwa karne nyingi, Magharibi imeinyonya dunia ya Kiislamu na kuyaweka mataifa yake chini ya shinikizo na dhulma. Mateso na mauaji yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ghaza yasingewezekana bila uungaji mkono wa Marekani; na mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran yasingewezekana bila idhini ya wazi ya Marekani na nchi za Magharibi.

Aliendelea kusema: Kwa hiyo, ni lazima tuwe waangalifu. Magharibi na Marekani zina historia ndefu ya njama na hila kwa karne nyingi. Mvutano wetu na Magharibi na Marekani ni mvutano kati ya mantiki ya uhuru dhidi ya mantiki ya utawala na udhibiti. Kinyume na madai yao ya kuionesha Iran kama tishio, kwa hakika wao wenyewe ndio tishio katika mfumo wa kidunia.

Kabriaei-Zadeh alisisitiza: Je, imewahi kushuhudiwa Iran ikivamia nchi nyingine? Ilhali utawala haram wa Kizayuni, katika muda mfupi wa uwepo wake mchafu, umefanya mashambulizi yasiyo na idadi dhidi ya wananchi wa Palestina na majirani zake.

Mshauri wa masuala ya kitamaduni wa Iran alikumbusha kuwa: Marekani imezivamia nchi nyingine mara mia kadhaa; ikiwemo Iraq, Afghanistan, na hivi karibuni Venezuela na Iran. Haya yote yanaonesha tabia ya kibeberu ya Marekani. Hata hivyo, wananchi wa Iran wamesimama imara dhidi ya tamaa na dhulma za maadui, na chini ya uongozi wa Mtukufu Ayatullah Khamenei, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, watawashinda maadui hao kwa hila na njama zao.

Chanzo: Idara ya Mahusiano ya Umma ya Shirika la Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha